March 04, 2016

Makamu Mwenyekiti wa Mhama cha Mapinduzi Zanzibar Dr. Ali Aohamed Ahein amelezea kusikitishwa na tukio la uripuaji wa bomu katika maskani ya kisonge Aichenzani mjini Zanzibar.
Dr. Shein ambae pia ni rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza Mapinduzi akiwa katika eneo la tukio amelitaka jeshi la polisi kuimarisha ulinzi na kuwakamata waliohusika na tukio hilo.
Amesema Serikali haiwezi kutetereka kwa vitendo alivyoviita vya kihuni vinavyotishia amani ya nchi na kujenga hofu kwa wananchi.
Dr. shein amesema vitendo hivyo haviwezi kusitisha na kutisha wananchi wasiweze kupiga kura katika uchaguzi wa marudio march 20 kukirudisha madarakani chama cha mapinduzi.
 


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia
  Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein,
(kushoto)  akizungumza na wanachama wa CCM na wapenda amani wakati
alipofika katika Maskani ya Kisonge Mjini Unguja leo kuangalia  hasara
iliyopatikana kutokana na mripuko wa bomu uliosababishwa na watu
wasiojuilikanwa jana usiku,[Picha na Ikulu.]

0 comments:

Post a Comment