February 06, 2016

Bodi ya Mapato Zanzibar  ZRB  inakadiria kukusanya kiasi cha shilingi Bilion 199 kupitia vyanzo mbalimbali vya mapato katika kipindi cha mwaka wa fedha 2016/17.
Afisa uendeshaji wa bodi hiyo Shaaban Yahya amesema fedha hizo zinategemea kukusanywa kutoka katika taasisi za serikali,   binafsi, vikosi maalum  na wafanyabiashara  wa viwango vya juu.
Amesema makadirio hayo ya ukusanyaji wa mapato yanapangwa na Wizara ya fedha kupitia vigezo  wanavyovipanga kulingana na ukuwaji wa mapato katika kila taasisi.
Afisa Yahya amefahamisha kuwa  ZRB vyanzo vyake vikuu vya mapato ni hoteli, usafiri wa baharini na anga, nishati, mawasiliano na kodi ya ongezeko la thamani.

Ameomba ushirikiano na taasisi mbalimbali kunufanikisha kazi hiyo pamoja na kuwasisitiza wananchi kudai risiti wakati wanapofanya manunuzi.

0 comments:

Post a Comment