February 06, 2016

Jeshi la Polisi Zanzibar limesema limejipanga kupambana na vitendo vya rushwa pamoja na kuongeza kasi ya utendaji kazi zake za kila siku.
Kamishna wa Jeshi hilo Hamdan Omar Makame amesema jeshi hilo amesema mara nyingi poolisi wamekuwa wakisemwa vibaya kwa vitendo vya askari wake kujihusisha na rushwa.
Akizungumza na maafisa na askari polisi wa Mikoa miwili ya Pemba huko Madungu Chake Chake  amesema mkakati huo umeandaliwa ili kujiimarisha kiutendaji na kupambana na v itendo hivyo.
Kamishna Makame amewataka askari hao kuongeza kasi ya utendaji katika kupambana na vitendo vya udhalilishaji wa kijinsia  vinavyo ongezeka kwa kasi Zanzibar.
Katika hatua nyengine ameelezea kufurahishwa  na  askari hao kwa kazi nzuri ya kusimamia uchaguzi wa 2015 uliofanyika katika hali ya amani na utulivu.

Kwa upande wao askari wa jeshi hilo wameomba kurekebishwa mfumo wa uwekaji kumbukumbu zao  kwani wamekuwa wakikosa haki zao kutokana na kukosekana kwa kumbukumbu zao muhimu.

0 comments:

Post a Comment