Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Taifa
Dkt Jakaya Mrisho Kikwete amesema chama hicho kimelazika kukubaliana na maamuzi
ya Tume ya uchaguzi Zanzibar ZEC kwa kuwa ndiyo yenye mamlaka ya kufanya hivyo.
Amesema CCM ilitamani kusingekuwepo na marudio
ya Uchaguzi visiwani Zanzibar kwa kuwa maandalizi ya kuuandaa ni kazi nzito na
inatumia gharama kubwa hadi kufanyika.
Tulikuwa tumejiandaa kushangilia, lakini Tume
wakasema kuwa uchaguzi unafutwa kwa kuwa kulikuwa na dosari kubwa, tukasikitika
sana lakini kwa kuwa tume wameamua, tukashauriana na wenzetu wa Zanzibar,
tukaona ni bora kukubali kurudia uchaguzi huo, lakini hatukupenda”
Amewaomba wanachama wa chama hicho Zanzibar kujiandaa kikamilifu
kushiriki uchaguzi huo wa marudio hapo 20 Machi 2016 kama
ilivyoelekezwa na ZEC kwani ndio njia pekee ya
kuiwezesha kupatikana demokrasia kufuatia ule wa awali kuwa na kasoro kadhaa.
Akizungumza katika maadhimsho ya kutimia miaka 39 ya kuzaliwa kwa
Chama Cha Mapinduzi Mkoani Singida Dkt Kikwete ambae pia ni
rais msataafu wa Tanzania amesmema chama hicho ndicho chenye uwezo
wa kusimamia mageuzi na mabadiliko ya kweli na kitaendelea
kuimarika na kukubaliwa na wananchi huku kikijihakikishia ushindi
mwaka 2020.
Nae Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe
Magufuli amewaagiza viongozi wa ngazi zote wakiwemo wa mikoa na wilaya kutumia vyeo
vyao katik kuhakikisha wanaondoa kero zinazowakabili wananchi kulingana na matakwa ya
ilani ya CCM inayochoongoza nchi kwa sasa.
Akitoa salam zake katika sherehe hizo, amesema tayari serikali
itaendelea kuyafanya kazi kikamilifu ikiwemo kuwabaini wazembe
na mafisadi "kutumbua majipu" kwa maslahi ya watanzania bila
kujali vyama vyao.
“Nawaeleza watendaji wote serikalini kuwa atakayeshindwa kufanya
kazi, nitamueleza kwa upole sana maana mimi ni mtu mpole, nitamuambia akae
pembeni apishe wengine”
Rais Magufuli pia ametumia nafasi hiyo kukishukuru Chama cha
Mapinduzi kufanikisha yeye kuwa Rais kwa kuwa bila chama hicho yeye
asingelipata nafasi hiyo.
“Nataka watanzania wote wajue kuwa bila CCM mimi
nisingekuwa Rais wao, kwa hiyo huwezi kunitenganisha mimi na CCM, ndiyo maana
leo nimekuja nimevaa kijani yangu hapa na sioni kama kuna chama kingine
chochote kitakachokuja kutawala Tanzania zaidi hiki”
Rais Dk. John Pombe Magufuli akiwapungia mikono
wana CCM
na wananchi wakati alipowasili kwenye uwanja
huo.
|
Baadhi ya wasanii wa Bongo Move
waliohudhuria katika maadhimisho
hayo kwenye uwanja wa Namfua mjini
Singida.
|
0 comments:
Post a Comment