February 07, 2016

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Ali Mohamed Shein amejumuika katika chakula maalum kwa Vijana walioshiriki Halaiki ya sherehe za Maadhimisho ya miaka 52 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
Akizungumza mara baada ya chakula hicho cha mchana kwa niaba ya Rais wa Shein Waziri wa Afisi Ya Ikulu na Utawala bora Dk Mwinyihaji  Makame amewataka  vijana kuelewana hasa katika kuendeleza maendeleo ya nchini  kwa misingi ya amani bila ya kurubuniwa na wasioipendelea mema Zanzibar.
Amefahamisha kuwa Serikali ipo pamoja na vijana wote katika kujenga upendo na maendeleo katika nchi.
Aidha Dkt Makame amesema hatua ya kula pamoja na vijana hao ni kujenga upendo kati ya viongozi wa juu na wanachama wa ngazi ya chini.
Amewataka  vijana kulinda na kuendeleza Mapinduzi ya Zanzibar  kwani ndio yaliyoung’oa ukoloni huko nyuma wanakotokea.
“Vijana ndio tegemeo kubwa tunalolinalotegemea hivi sasa la kuendeleza mapinduzi yaliyokuwepo , hivyo ipo haja ya kuisoma historia ya nchi hii ili muweze kuyajua kwa undani ili vizazi vinavyokuja viweze kufaidika “, alisema.

Vijana walishiriki katika hafla hiyo ya chakula cha mchana iliyoandaliwa na Dkt Shein kwa kufanikisha shereha za miaka 52 ya Mapinduzi zilizofanyika hivi karibuni ni pamoja na kundi la chipukizi CCM, kikundi cha uhamasishaji pamoja na Veterani wa Young Pioneers.


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi
Dk.Ali Mohamed Shein (wa pili kushoto) na Makamo wa
Pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi wakitia chakula
katika hafla aliyowaandalia Vijana wa Halaiki ya sherehe za
miaka 52 ya Mapinduzi ya Zanzibar iliyofanyika katika
viwanja vya ukumbi wa Salama Bwawani Mjini Unguja,

Baadhi ya Vijana walioshiriki katika halaiki  ya maadhimisho ya
 Sherehe za Miaka 52 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar  wakila
Chakula  katika hafla ya iliyoandaliwa na  Rais wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein.
 [Picha na Ikulu.]

0 comments:

Post a Comment