Jeshi
la Polisi visiwani Zanzibar kwa kushirikiana na kitengo cha polisi wa kimataifa
Interpol na kampuni ya kimataifa ya ushauri wa kulinda Alama za biashara
Brand Protection Agency linaendelea na uchunguzi kuhusu Kontena lenye
urefu wa futi 40 lenye DVD 1,0310 zisizokidhi viwango ambazo zinadaiwa
kubeba jina la SINGSUNG.
Kontena
hilo ni lenye namba PCIU888100 (1) Seal Namba T. 093094 PIC
lililosafirishwa na meli ya MV. Kota Harmut kutoka nchini
China lilikamatwa katika bandari ya Zanzibar.
Akizungumza na wanahabari visiwani Zanzibar wakati akitowa taarifa ya
matukio mbali mbali Naibu mkurugenzi wa upepelelezi wa makosa ya jinai
Zanzibar Salum Msangi amesema kuwa upelelezi utakapokamilika watafikisha kesi
hiyo mahakamani kuendelea na utaratibu ikiwa lengo ni kutokomeza bidhaa zisizo
na viwango na kuifanya nchi kama jaa la bidhaa mbovu.
Aidha
kamanda Msangi amesema kuwa pamoja na hali hilo wanaendelea kumshikilia
Mtu mmoja anaedaiwa kutowa CLIP yenye lugha za matusi dhidi ya Rais wa Zanzibar
na mwenyekiti wa baraza la mapinduzi Dr Ali Mohammed Shein katika mitandao ya
kijamii huku wakiendelea kuwafuatilia wengine ambao wameeleza wanawafahamu.
Amesisitiza
upana wa demokrasia isiwe sababu ya kufanya uhalifu na jeshi lipo macho zaidi
kwa watu hao
Aidha
kamanda amezungumzia njia mpya ambayo inatumika kusafirishia madawa ya kulevya
hasa pale walipokamata kasha 3 zenye ukubwa tofauti zenye uzito wa kilo 18
zilizotoka Adisababa Ethiopia zenye majani ambayo kiutafiti yakiwekwa katika
maji hugeuka na kuwa mirungi.
Pamoja
na mambo mengine amevitaka vyombo vya habari kuendelea kufanya utafiti wa
habari zao kwa kila kilichojitokeza baadhi ya vyombo hutowa taarifa
zisizo sahihi.
0 comments:
Post a Comment