Jaji Mkuu wa Zanzibar Jaji Omar Othman Makungu
amesema mbali na makosa ya mitandao yanafanywa na watu kadhaa Zanzibar bado mahakama
haina uwezo wa kuyashughulikia kutokana sheria ya makosa hayo Tanzania
haijaanza kutumika rasmi.
Amesema sheria hiyo iliyopitishwa na Bunge la Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania ili iweze kufanya kazi Zanzibar lazima iridhiwe na
baraza la Wawakilishi.
“ Hili suala bado hadi sasa halijafanyika ndo
tunasubiri wapitishe ili tuweze kuanza kuzishughulikia kesi za aina hiyo na
kuzitolea hukumu”. amesema Jaji Makungu.
Alikuwa akizungumza na waandishi wa habari
kuhusu maadhimisho ya siku ya sheria yanayofikia kilele chake Februari 10, 2016
yakiwa na kauli mbiu Matumizi mabaya
ya mitandao ya kijamii yanaweza kuwa chanzo cha uvunjaji wa sheria na amani ya
nchi..
Jaji makungu amesema sheria
hiyo imeanza kutumika Septemba 1, 2015 wakati Baraza la Wawakilishi lilikuwa limeshavunjwa
na hivyo kulikuwa na ugumu kuridhiwa.
Akizungumzia kuhusu maadhimisho hayo kwa Zanzibar
yataambatana na uwekwaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa
mahakama mpya ya watoto huko Mahonda pamoja na kuifanyia matengenezo mahakama
kama hiyo huko Pemba.
0 comments:
Post a Comment