Rais Dk John Pombe Magufuli
amelihutubia taifa kupitia wa Wazee wa Dar e salaam amesema serikali
haitamvumilia mtu atakaehatarisha amani ya nchi pamoja na kuwatahadharisha viongozi
na wananchi wengine kuhusu ubadhirifu wa mali ya umma.
Katika hotuba yake hiyo ameainisha changamoto
kadhaa zinazolikabili taifa na mikakati inayochukuliwa na Serikali ya awamu ya
tano kupambana nayo pamoja na kuwaahidi wananchi kuwatumikia na kukabili
matatizo yao.
Akizungumza na wazee hao wa Dar es salaam
katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini humo, Rais Dk John Pombe Magufuli
amewahakikishia Watanzania kwamba Serikali ya awamu ya tano amezungumzia kuhusu
hali ya kisiasa visiwani Zanzibar na kueleza ni vigumu yeye kuingilia maamuzi
ya tume ya taifa uchaguzi Zanzibar ambayo ni huru.
“ Napenda kuheshimu sheria na ZEC ina uhuru wa
kuamua mambo yake lakini kama kuna tafsiri mbaya, na mahakamani zipo sasa unamwambia Magufuli aingilie
nini….. Jukumu langu kama amiri
jeshi mkuu ni kuhakikisha amani ya Zanzibar inaimarika, yeyote atakaeleta fyoko
fyko ajue vyombo vya usalama vipo” amesema Rais magufuli.
ZAIDI HII HAPA HOTUBA KAMILI
SIKILIZA
0 comments:
Post a Comment