Kitengo cha ufuatiliaji nyendo za maradhi kimesema
kuna uwezekano wa Zanzibar kuwa na ugonjwa wa zika kutokana na mbu
wanaoambukiza ugonjwa huo wa aina ya AEDES AEGYPTI anapatikana visiwani humo.
Mkuu wa kitengo hicho Dkt Salma Masauni Yusuf
amesema hadi sasa hakuna mgonjwa
alibainika kuambukizwa ugonjwa huo.
Amesema mbu huyo anaishi kwenye mazingira machafu
kama mbu wa malaria na kwamba huuma zaidi nyakati za mchana tofauti na mbu wa
malaria ambae anaumwa usiku.
Dkt Salma amesema waathirika wakubwa wa ugonjwa huo ni
mama mjamzito na anapoambukizwa ugonjwa wa zika huzaa mtoto mwenye kichwa
kidogo na ubongo mdogo na hadi sasa hauna tiba wala tiba ispokuwa mgonjwa hutibiwa
dalili za maradhi yanayomsumbua.
Hata hivyo amefahamisha kuwa watoto wenye vidogo
waliozaliwa Zanzibar hawakusababishwa na ugonjwa wa zika kutokana na uchaguzi
walioufanya.
Mkuu huyo wa Kitengo cha ufuatiliaji nyendo
za maradhi ameeleza kuwa kitengo chake kupitia wizara ya afya imeimarisha
huduma za maabara ili kuchunguza ugonjwa wa zia kwa hatua za awali.
Amesema mbu huyo anaweza kuambukiza mwanamke moja
kwa moja au kupitia kwa mwanamme aliyeambukizwa kupitia tendo la ndoa.
“ Utafiti umethibitisha kwamba mwanamke anaweza
kuambukizwa ugonjwa wa zika kupitia kwa mwanamme mwenye ugonjwa wa zika anaweza
kuambukizwa mkewe kupitia damu kwa kufanya tendo la ndoa” amesema Dkt Salma.
Amefahamisha kuwa kirusi cha zika kinaweza
kugundulika kuanzia siku moja hadi saba na baada ya hapo mgonjwa anaweza kupata
matatizo ya ubongo na miguu kupooza na wajawazito hujifungua watoto wenye
vichwa vidogo.
Amesema kitengo hicho kitaendelea kutoa elimu kwa
wagonjwa wanaofika hospitali na vituo vya
afya ili kuchukua hatua za kujikinga na ugonjwa huo pamoja na kuwapima wageni
wanaoingia nchini kupitia uwanja wa ndege na bandarini.
Kuhusu dalili za ugonjwa huo Dkt Salma amesema
amesema ni pamoja na kuumwa na kichwa, maumivu ya viungo, macho kuwa mekundu na
kupata vipele vidogovidodo kama harara.
0 comments:
Post a Comment