February 24, 2016

Wizara ya Kilimo na Maliasili Zanzibar imesema kuna hatari ya kuwepo mavuno kidogo ya mpunga katika msimu huu kufuatia uchelewaji wa matayarisho ya mashamba kwa ajili ya kilimo hicho.
Naibu katibu mkuu wa kilimo Juma Ali Juma amesema  maeneo mengi ya mashamba hayo hayajafikiwa na kutokana na wakulima kushindwa kuchangia huduma za matrekta.
Amewaambia waandishi wa habari kuwa  katika msimu huu wa kilimo wanatarajia kulima ekari elfu 33 lakini hadi sasa ni ekari elfu tisa pekee ndio zimehudumiwa katika vijiji vya mtende na muyuni mkoa kusini Unguja.
Amesema ingawa wizara hiyo inakususida kutoa pembejeo kwa wakulima ikiwemo mbolea, dawa za kuulia magugu na mbegu lakini bado mwamko wa wakulima ni mdog.

Katika hatua Wizara ya Kilimo na Maliasili imeandaa mkakati wa kurejesha kilimo cha asili kisichotumia dawa na mbolea zenye kemikali ikiwa ni juhudi za kuimarisha kilimo cha asilia Zanzibar.

0 comments:

Post a Comment