Chama
cha Wakulima (A.F.P) kimesema kitashiriki uchaguzi wa marejeo wa Zanzibar huku kikilaani watu wanaotaka kufanya fujo siku ya kufanyika uchaguzi huo tarehe 20 machi mwaka
huu
Hayo
ameyasema na Mgombea wa Urais wa chama hicho Said
Suod huko Vuga Mjini Zanzibar katika ukumbi wa Cultuer wakati akizungumza na
waandishi wa habari kuhusu tamko la kushiriki
kwa uchaguzi kwa ngazi zote.
Amesema
chama chake kitashiriki uchaguzi bila yakufanya fujo na kuheshimu sheria zote
zilizowekwa katika uchaguzi ili kuweza kufanikisha kufanyika uchaguzi huo kwa amani.
Amesema
kuwa uchaguzi uliofanyika tarehe 25/10/2015. Ulifutwa kihalali kutokana na
udanganyifu uliofanyika . na kupelekea kuhairishwa kwa uchaguzi huo na kutajwa tarehe ya kurejewa uchaguzi.
Hata
hivyo amefahamisha zaidi watu waliosababisha udanganyifu na kupelekea kufutwa
kaw uchaguzi ni vyema wakachukuliwa hatua ili wasijerejea kutokea kwa
ubadhilifu mwengine.
Aidha
amewaomba viongozi wakuu wa Serikali kuzidisha ulinzi siku ya uchaguzi li
kuweka utulivu katika nchi na kuepusha kutokea kwa vurugu zitakazo sababish
uvunjifu wa amani
Sambamba
na hayo amewaomba wazanzibar wote kushiriki uchaguzi na kuwachaguwa wagombea kwa
ngazi zote za udiwani, urais na uwakilishi bila kuleta fujo ya aina yoyote.
:Maelezo Zanzibar.
0 comments:
Post a Comment