Hali ya Sintofahamu imetawala Bungeni jioni hii kufuatia wabunge
wa Upinzani kupinga TBC kusitisha kurusha live matangazo ya moja kwa moja
kuanzia jana kwa kigezo cha kubana matumizi.
Kutokana na vurugu hizo, Polisi wamelazimika kuingia Bungeni na
kuwatoa nje wabunge wa Upinzani kufuatia kugoma kutokana na maagizo ya
Mwenyekiti wa Kikao cha Bunge, Andrew Chenge.
Chanzo cha vurugu hizo ni Wabunge wa Upinzani kupinga
kuendelea kwa mjadala wa Bunge wakitaka kauli ya Waziri wa
Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo, Nape Nnauye kuhusu TBC kusitisha kurusha
matangazo ya moja kwa moja toka Bungeni ijadiliwe kwanza.
Sakata hilo liliibuka tangu asubuhi ambapo Mwenyeki wa Bunge,
Andrew Chenge aliahirisha Kikao cha Bunge mara mbili huku akiitaka kamati ya
uongozi kukutana ili kutoa majibu.
Maamuzi ya kamati ya uongozi
Baada ya Bunge kurejea jioni hii mwenyekiti wa Bunge Andrew Chenge
ameliambia Bunge kuwa maamuzi ya kamati ya uongozi baada ya kuketi mchana wa
leo ni kama ifuatavyo.
(a) Mwenyekiti wa Bunge alikuwa sahihi kutaka hoja iliyokuwa mbele ya Bunge kuhusu hotuba ya Rais iendelee.
(a) Mwenyekiti wa Bunge alikuwa sahihi kutaka hoja iliyokuwa mbele ya Bunge kuhusu hotuba ya Rais iendelee.
(b) Hakuna haki yoyote ya Bunge iliyovunjwa kwa Bunge kuendelea na
kazi yake baada ya hoja ya Waziri
(c) Hoja ya Bunge iliyo mbele ya Bunge ni hotuba ya Rais na kamati
ya uongozi imeagiza shughuli ziendelee kama kawaida.
(d) Endapo kuna Mbunge yoyote ambaye hataridhika atumie kanuni ya
5 (4) kuomba kibali kwa katibu wa bunge ili apate nafasi maalumu.
Aidha kwa mujibu wa ratiba ya kikao cha Bunge ni kwamba Bunge
litajadili hotuba ya Rais Magufuli aliyoitoa wakati wa ufunguzi wa Bunge la 11
Novemba 20, 2015 kwa muda wa siku 3. Baada ya kauli hii, vurugu ziliibuka
Bungeni
Wabunge wa Upinzani walianza kupiga mayowe, ikiwemo
kuimba nyimbo mbalimbali suala lililomlazimu Mwenyekiti kuwaondoa Wabunge wa
Ukawa wote watoke nje ili wabunge wengine waendelee na kikao cha kujadili
hotuba ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli.
Wabunge wa CCM waliendeleaa na kikao cha Bunge.
0 comments:
Post a Comment