Waziri mkuu, Kassim Majaliwa amefanya tena ziara ya kushtukiza bandari
ya Dar es Salaam na Shirika la reli
Tanzania TRL na kubaini upotevu
wa makontena zaidi ya 2431.
Akiwa bandarini hapo amekagua mfumo wa utoaji na uingizaji
mizigo akiwa na ripoti ya ukaguzi inayoonyesha majina ya waliopitisha makontena
hayo bila kulipiwa kodi.
Katika maongezi ya awali alihakikishiwa kuwa mfumo hauruhusu
kontena kuibiwa lakini waziri mkuu aligundua hali hiyo.
Kufuatia hali hiyo ametoa muda wa masaa matatu hadi saa kumi na
mbili jioni leo apewe tarifa dhidi ya hatua zilizochukuliwa kwa wahusika.
Alipotembelea shirika la reli waziri mkuu majaliwa amegundua mabilioni
ya fedha zimetumika na miradi iliyokusudiwa bado haijatekelezwa.
0 comments:
Post a Comment