Rais wa Jamhuri ya
Muungano Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli ametoa siku saba kwa wafanyabiashara walioingiza mizigo kwa
kukwepa kodi kulipa mara moja kodi kwani watachukuliwa hatua kali za kisheria.
Ametoa agizo hilo leo
Ikulu jijini Dar es Salaam alipokuwa na mkutano na wadau wa sekta
binafsi kuwasikiliza maoni yao ikiwa ni sehemu ya ahadi zake katika
kipindi cha kampeni za kuomba kura za kiti cha Urais,lengo likiwa ni kukuza
uchumi wa nchi kupitia sekta binafsi.
Amesema ni lazima wadau
hao kuweka maslahi ya taifa mbele ili kuweza kujenga taifa lenye maendeleo
makubwa ya kiuchumi.
Rais Magufuli ameendelea
kusema kuwa katika kipindi hichi cha miaka mitano amedhamiria kuijenga nchi na
watu wasimuelewe vibaya kwa maamuzi anayofanya kwani ni kwania njema ya kuleta
maendeleo.
Pamoja na hayo Mheshimiwa
Dkt.Magufuli ameaahidi kutoa ushirikiano kwa wadau wa sekta binafsi hasa
wazalendo kwa vile wanamchango mkubwa katika
kukuza uchumi.
Kwa upande wa Mwenyekiti
wa Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF) Regnald Mengi amemuomba Rais Magufuli kuendelea kukemea masuala ya
rushwa pamoja kusaidia kupunguza utitiri wa kodi Tanzania.
0 comments:
Post a Comment