Klabu ya Waandishi wa habari kisiwani Pemba, Pemba
Press Club -PPC imelaani kitendo cha kuchomwa moto kwa kituo
cha Radio cha Hist FM kilichopo Migombani Mjini Unguja hivi karibuni.
Kituo hicho kilichomwa moto desemba 2 majira ya 7:30 baada ya watu zaidi ya 15 kukivamia wakiwa na silaha huku wamejifunika
nyuso na kusabisha hasara inayokadiriwa kuwa ni zaidi ya shilingi milioni 70.
Katibu wa klabu hiyo Khatib Juma Mjaja amesema
wanahabari wa Pemba, hawafurahishwi na vitendo vyovyote vya kuhujumu au
vinavyokwaza uhuru wa habari kwa namna yoyote ile kwani haki ya habari ni
miongoni mwa haki muhimu zinatambuliwa na katiba ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania ya 1977 na katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984.
Amesema kitendo hicho kimelenga kukwamisha
demokrasia ya habari kwa jamii ya Zanzibar na Tanzania kwa ujumla.
PPC imeziomba taasisi zinazohusika kulifanyia kazi
suala hilo na sheria kuchukuwa mkono wake kwa wote watakaobainika mkuhusika na
kitendo hicho dhalimu.
“kile ni kitendo cha kinyama na kinapaswa kulaniwa
na kila mtu, kinasikitisha sana na kimeweza kurudisha nyuma maisha ya watu,
watu wanategemea kuendesha familia zao pale halafu wanakwamishwa na watu wachache”amesema.
Amesema
tasnia ya habari imekuwa kihimiza maendeleo ya nchi, ikiwemo vijana kujiajiri
wenyewe na kutokutegemea ajira kutoka serekalini, amevitaka vilabu vya habari
kuwa mtari wa mbele kukisaidia kituo hicho kwa hali namali.
0 comments:
Post a Comment