Waalimu Nchini wametakiwa kuwapa fursa na kuwahamasisha
wanafunzi kushiriki katika michezo ili kuwezesha kupata timu nzuri
na kushiriki katika mashindano ya Kimataifa.
Hayo yameelezwa na Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya
Michezo Wizara ya Habari Utamaduni Wasanii na Michezo Tanzania Leona Tadeo
alipokua akifunga Shamrashamra za Tamasha siku ya Walimu Duniani katika
Uwanja wa Amani mjini zanzibar.
Amesema nchini Tanzania wananchi wengi wanalamika kwa
kutofanya vizuri katika michezo kutokana na kukosekana vijana waliojengeka
kimichezo tangu wadogo jambo linalorejesha nyuma maendeleo ya michezo
hiyo.
Amesema jukumu hilo kuwajenga wanafunzi kimichezo linapaswa
kutekelezwa na waalimu wakati wapo watoto wakiwa skulini.
Kwa upande wake mwalimu Mussa Abdulrabi kutoka
Wizara ya Elimu amesema lengo la tamasha hilo ni walimu kushiriki michezo
mbalimbali ili kuonesha vipaji vyao katika michezo hiyo.
Sambamba na hayo mwalimu huyo ameaahidi kuwa watawashajiisha
walimu wenzao kwenda kujiunga na Chuo cha Maendeleo ya Michezo ili
kupata walimu wengi ili kuungana nia ya Serekali katika kuendeleza
Michezo .
Katika shamrashamra hizo kumefanyika michezo ya kuvuta kamba,
Mpira wa Mkono, mbio za Gunia pamoja na Mpira wa miguu iliyowshirikisha
walimu kutoka Mkoa Kusini Unguja, Mkoa wa mjini Magharib na Mkoa wa Kaskazini.
Maelezo Zanzibar
0 comments:
Post a Comment