Mufti mkuu wa Tanzania, Sheikh
Abubakar Zuberi, amewakosoa baadhi ya masheikh walioshindwa kuwajibika na
kusema watu kama hao wanawatia aibu waislamu.
Akizungumza mjini dar es
salaam amewataka viongozi wa Baraza kuu la waislamu Tanzania BAKWATA kubadili
fikra na mienendo yao katika utendaji ili iwe dira kwa waislamu.
Amesema bakwata ina sura
mpya na malengo makuu ni kuwaunganisha waislamu, na kusisitiza kuwa, umoja
waumini hao utasaidia kuwa na nafasi muhimu katika masuala ya
kitaifa.
Mufti mkuu ameongeza pia BAKWATA
itaanzisha kitengo cha masuala ya uchumi kitakachoongozwa na wataalamu
watakaokuwa na jukumu la kuiandaa jamii ya kiislamu kushiriki kukuza uchumi wa
nchi.
Mufti zuberi ameanza ziara
ya kuzunguka nchi nzima kuhamasisha umoja na mshikamano miongoni mwa waislamu.
0 comments:
Post a Comment