Waziri wa habari, Utamaduni, sanaa
na michezo Nape Moses Nnauye amewatoa hofu wamiliki wa Vyombo vya Habari nchini
hususani Magazeti pamoja na wanahabari kuwa atahakikisha anakuwa mlezi wa
vyombo vya habari pamoja waandishi wa habari ili vifanye kazi kwa umakini.
Akizungumza na watumishi na wakuu wa
taasisi za wizara hiyo jijini Dar es salaam mara baada ya kuwasili katika afisi
za wizara hiyo Nape amesema kuteuliwa nafasi hiyo isiwatie hofu kuwa
atautaathiri muhimili huo wa habari.
Amesema ufinyu wa bajeti ni miongoni
mwa changamoto zinazoikabili wizara hiyo hivyo amesema atahakikisha
anaibana serikali ili kuongeza bajeti kwa wizara hiyo kwa lengo la kutekeleza
majukumu yake vizuri.
Naibu
waziri Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo
Anastazia
James Wambura (kushoto) akimkaribisha waziri wa wizara hiyo
katika
ofisi za wizara hiyo leo jijini Dar es Salaam.
|
0 comments:
Post a Comment