December 14, 2015

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
Akisalimiana  na Balozi wa Japan nchini Masaharu Yoshida aliyefika
Ikulu Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya mazungumzo. Katika Mazungumzo hayo
Balozi Yoshida amempongeza Rais Magufuli kwa kuchaguliwa
kuiongoza Tanzania na pia amezungumzia miradi mbalimbali
inayofadhiliwa na Japan hapa nchini.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiagana na  Balozi wa Cuba nchini Tanzania,
Mhe. Jorge Luis Lopez, baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika
 Ofisini kwa Mhe Makamu, Ikulu jijini Dar es Salaam,
leo Desemba 14, 2015 kwa mazungumzo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiagana na  Balozi wa Uturuki nchini Tanzania,
Mhe. Yasemin Eralp, baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika
Ofisini kwa Mhe Makamu, Ikulu jijini Dar es Salaam,
leo Desemba 14, 2015 kwa mazungumzo.

0 comments:

Post a Comment