Katibu mkuu afisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais
Dkt Omar Dadi Shajak amesema uchumi wa Zanzibar pekee hauwezi kukabiliana na
athari za mabadiliko ya tabia nchi.
Amesema ili kutekeleza
maazimio yaliyofikiwa katika mkutano wa kimataifa wa hali ya hewa uliofanyika
mjini Paris Ufaransa hivi karibuni Zanzibar inahitaji kuungwa mkono na jumuiya na mashirika ya kimataifa
ili kukabiliana na hali hiyo.
Akizungumza katika
mkutano na kamati ya uongozi ya mabadiliko ya tabia nchi Dkt shajak amesema
tayari Zanzibar ina maeneo 147 yaliyoathirika hivyo kuna haja ya kuunga mkono maazimio yaliyofikiwa katika
mkutano huo.
Nae Mkurugenzi mkuu wa
mamlaka ya usimamizi wa mazingira Zanzibar Sheha Mjaja Juma miundo mbinu mingi
inaweza kupotea na kuharibika kwa iwapo juhudi za makusudi hazitachukuliwa na
wadau wa mazingira.
Amesema kinachopaswa ni kuandaliwa
program mbali mbali za kuhimili mabadiliko ya tabia nchi ikiwa ni pamaoja na
kutoa elimu kwa jamii na uwezo wa kifedha teknologia.
Kwa upande wake Afisa
mazingira kutoka ofisi wa Makamu wa kwanza wa Rais Soud Mohamed Juma amewataka
wananchi kupunguza vitendo vya kukata miti ovyo na kuharibu rasilimali kwa
kiwango kikubwa.
0 comments:
Post a Comment