December 06, 2015


Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar imesisitiza kuwa haitolipa fidia yeyote kwa wananchi Fuoni Zanzibar waliovunjiwa nyumba na maduka kwa ajili ya utanuzi wa  barabara.
Ujuenzi wa barabara hiyo kuanzia Mwanakwerekwe makaburini hadi Fuoni kituo cha polisi umekuwa unasusua kutokana na baadhi ya wananchi kukaidi amri ya kuvunja kwa hiyari nyumba zao.
Kauli hiyo ameitoa Katibu mkuu wa Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano Dkt Juma Malik Akil akiwa na Mkuu wa wilaya Ya Magharib B Ayoub Mohammed Mahmoud pamoja injinia Cosmas wakati wakisikiliza malalamiko ya wananchi hao.
Amesema mradi huo upo kihalali na umefuata sheria zote na mwananchi yeyote mwenye malalamiko aende na hati zote ili sheria ifuate mkondo.
Amefahamisha kuwa sheria ya barabara inasema kuwa si ruhusa mtu yoyote kujenga ndani mita 15 za barabara na kama yupo aliyjenga ndani ya eneo hilo anapaswa kuvunja nyumba yake ili mjenzi wa barabara hiyo akabidhiwe eneo la ujenzi kuanza kazi mara moja.
Ujenzi wa barabara hiyo kuanzia Mwanakwerekwe makaburini hadi Fuoni kituo cha polisi unatarajia kutumia zaidi ya shilingi bilioni tano zinatakazotolewa na serikali.



0 comments:

Post a Comment