Rais wa Zanzibar na
mwenyekiti wa baraza la mapinduzi Dkt Ali Mohamed Shein ameizinuda meli mpya ya
MV Mapinduzi II iliyonunliwa na Serikali bandarini mjini Zanzibar.
Meli hiyo
imetengenezwa na kampuni ya Daewoo nchini Korea ya kusini imewasili Zanzibar wiki iliyopita ya
Disemba 2, 2015 imegharimu dola za kimarekani milioni 30.6
ina uwezo wa kuchukua abiria 1200 tani 200 za mizigo.
Akizingumza katika
uzinduzi huo Rais Shein amesema serikali imeamua kuinunua meli hiyo ili
kuipunguzia majanga yanayoikumba Zanzibar kutokana na kuwepo meli chakavu
zilizokuwa ziwahudumia wananchi.
Amesema MV Mapinduzi II ni
bora na mpya na hakuna ulaghai wa kuidanganya serikali ulifanyika wa kuiuzia
meli iliyokuwa imeshatumika.
“Wananchi Msisikilize maneno ya mitaani kuwa hii Meli imeshatumika
suala hilo halina ukweli,”. Amesema Dkt Shein.
Amefahamisha kuwa
serikali kwa sasa imeamua kuimarisha sekta ya usafiri wa baharini kwa
kulifanyia mageuzi Shirika la meli ili lifanye kazi ya biashara yenye tija kwa
vile ni sekta hiyo ndiyo nyenzo muhimu ya kuongeza pato la taifa.
Dkt Shein ameongeza kuwa kwa
sasa Serikali
inategemea kuanza ujenzi Bandari kubwa ya mizigo eneo la Maruhubi mpiga duri na
tayari imeshaanza makubaliano na Serikali ya China kuanza ujenzi huo kuanzia
mwaka ujao ikiwa ni juhudi za kuimarisha sekta ya usafirishaji wa baharini.
0 comments:
Post a Comment