Jeshi la Polisi Nchini limeelezea faraja yake kutokana na mfumo
wa Viongozi wa Kitaifa kuonyesha muelekeo wa kuwajali watumishi wao kutoka
Taasisi tofauti za Umma na hata binafsi hasa wale watumishi wa ngazi ya
chini.
Afisa wa Polisi S.P Zakaria Benard ameeleza hayo alipokuwa akitoa shukrani za Jeshi hilo kwa Makamu wa Pili wa
Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi aliyefika katika Kata ya Goba Wilaya ya
Kinondoni Mkoa wa Dar es salaam kutoa mkono wa pole na kuifariji Familia
ya Koplo Yesaya Mwakambi aliyefariki Dunia kwa ajali ya Piki pili Ubungo Jijini
Dar es salaam.
Koplo Yesaya ni miongoni mwa Askari wa Usalama Bara barani wa
Jeshi la Polisi Nchini wanaowajibika kuiongoza Misafara ya Viongozi Wakuu wa
Kitaifa akiwemo wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alipata ajali akiwa
kazini mwezi Mmoja na nusu uliopita .
Kamanda Zakaria amempongeza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
Balozi Seif kwa uamuzi wake wa kutenga muda kwa lengo la kuifariji Familia ya
Koplo Yesaya.
Akitoa shukrani kwa niaba ya wanafamilia wa Koplo huyo Mchungaji
Isaya Isaleka ameiomba Serikali kuangalia uwezekano wa kuisadia Familia ya
Marehemu Koplo Yesaya Mwakambi ili iweze kuwa na nguvu za kukabiliana na maisha
yao ya baadaye.
Mapema Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar akiifariji familia
hiyo inayoongozwa na Mke wa Marehemu Bibi Wema Sanga amewataka kwa kuwa na moyo wa subira hasa Mkewe Mama wa watoto wawili Bibi Wema Sanga kwa kuondokewa na mpendwa wao.
Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
4/12/215.
0 comments:
Post a Comment