December 28, 2015

WATU 360 wameripotiwa kufariki dunia kutokana na ajali 4,291 za barabarani, zilizotokea Zanzibar kuanzia  mwaka 2008 hadi mwezi Disemba mwaka 2014.
Katika kipndi hicho cha miaka saba pia watu wengine 3,195 wamejeruhiwa katika ajali hizo.
Kwa mujibu wa Ripoti zinazotayarishwa kila mwaka na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), kwa kushirikiana na Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar (ZLSC), zinaonyesha matukio hayo ya vifo vya ajali za barabarani yanaongezeka kila mwaka.
Ripoti ya mwaka 2008 imeonyesha kuwa, jumla ya watu 48 walipoteza maisha na 409 walijeruhiwa na mwaka uliofuata (2009) walifikia 54, mwaka 2010 walipungua hadi 52 na mwaka 2011 watu hamsini  50 waliofariki.
Aidha miaka miwili iliofuta kulipungua na kufikia watu 39 na 29 kwa mwaka 2013 wakati mwaka 2014 iadi hiyo ilifikia watu 88 na majeruhi 547.
Aidha kutokana ripoti hizo za kipindi cha miaka saba iliopita mwaka jana ndio ulioripotiwa ajali nyingi, zilizofikia kufikia 845, huku mwaka 2010 zikifikia 692 na mwaka 2011 kuripotiwa ajali za barabarani 615
Kwa mujibu wa ripoti hizo, sababu kuu ya ajili hizo ni mchanganyiko wa matumizi ya barabara kati ya watembea kwa miguu, waendesha vyombo vya magurudumu mawili na gari za kawaida.
Sababu nyengine ni ubovu na uchakavu wa barabara katika maeneo kadhaa ya Zanzibar, udogo wa upana wa barabara, utekelezaji mbaya wa sheria za usalama barabarani na uendeshaji wa uzembe.
Haji Nassor, Pemba

0 comments:

Post a Comment