Vipodozi hivyo ni pamoja na Movet Crèame kutoka nchini Italia
na Medical Fade Crème kutoka Marekani vyenye uzito wa tani tatu vilikuwa yamechanganyishwa
na vitu vingine katika Makontena bandarini hapo.
Akitoa taarifa kwa
waandishi wa habari Mkaguzi wa Bodi hiyo Nassir Buheti amesema vipodozi hivyo vimepigwa
marufuku kutokana na kuwa Viambata vyenye kemikali vinavyoweza kuleta madhara
Mtumiaji ikiwemo ugonjwa wa saratani, Ulemavu pamoja na uharibifu wa ngozi.
Amefahamisha kuwa mawakala wa vipodozi hivyo wamedai kuwa
havikukusudiwa kuingizwa nchini wakati vimepigwa marufuku dunia nzima.
Mkaguzi Buheti amesema sheria ya Chakula, Dawa na Vipodozi ya mwaka 2006 inasema si
ruhusa kuingiza, kuuza, kusambaza vipodozi haramu na kuwataka wafanyabiasha wa
vipodozi, dawa pamoja na Chakula kutofanya udanganyifu wa bidhaa wanazoingiza
ili kuepuka madhara yasiongezeke nchini.
0 comments:
Post a Comment