Mwanasheria Mkuu wa
serikali ya Tanzania, George Masaju
amepinga hoja zilizoibuliwa na UKAWA kuhusu uhalali wa rais wa serikali
ya mapinduzi ya Zanzibar, Dkt Shein, kuhudhuria kwenye uzinduzi wa Bunge.
Amesema kuwa tayari Tume ya uchaguzi ya
Zanzibar ZEC imefuta uchaguzi, na kwa kuwa hakuna mtu
yeyote alieapa kiapo cha urais tofauti na rais wa sasa wa Zanzibar, Dkt Shein.
Hivyo
Dkt Shein anatambulika kama rais wa Zanzibar na ana uhalali wote wa kuhudhuria
katika uzinduzi wa Bunge la 11 huku akivitaja vifungu mbalimbali vya katiba ya Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania ya 1977 na katiba ya Zanzibar 1984.
Masaju ametumia ibara
ya 102 ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupangua hoja hizo inayoeleza
kuwa, kutakuwa na serikali ya Zanzibar itakayo julikana kama serikali ya Mapinduzi
ya Zanzibar itayokuwa na mamlaka katika Zanzibar juu ya mambo yote yasiyo mambo
ya muungano kwa mujibu wa masharti ya katiba hii.
Pia ametumia katiba ya
Zanzibar ya mwaka 1984 katika Ibara yake ya 26 ambayo inasema, kutakuwa na rais
wa Zanzibar ambae atakuwa mkuu wa nchi ya Zanzibar, kiongozi wa serikali ya
mapinduzi ya Zanzibar na mwenyekiti wa baraza la mapinduzi.
0 comments:
Post a Comment