Rais wa
Jamuhuri Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli amelihutubia bunge kwa mara
ya kwanza huku akiwataka watanzania kuwa serikali yake itatenda haki kwa kila
mtanzania.
Amesema pia haitafumbia macho wale wenye nia mbaya ya kuvuruga amani kwa
kuwa serikali inalengo la kuwatumikia wananchi ili kuindokana na ukata wa
umasikini.
Ametaja
vipaumbele vya serikali yake ni pamoja na kupunguza urasimu kubana matumizi
serikali, kurejesha nidahmu ya serikali na uwajibikaji kwa watumishi wa umma na
viongozi kwa ajili ya kuwatumikia wananchi.
Dk.Magufuli ameapa kuwashugulikia wala rushwa na mafisadi bila
kuwaonea haya ya aina yoyote kwani ndio wanaorudisha nyuma maendeleo ya taifa
kwa kutumia raslimali ya watanzania vibaya na kuomba bunge,Takukuru na wananchi
wenyewe kumuunga mkono.
“Nasema hili kwa kuwa anadhanira ya kweli ya kuifanya Tanzania iwe nchi
ya kipato cha kati”Dk.Magufuli
amesema.
Ameeleza kuwa kiu yake ni kuhakikisha uchumi wa kipato cha kati
unafanana na maisha ya wananchi wa Tanzania ili wafurahie matunda ya taifa lao
kwa kuimarisha sekta ya viwanda.
Katika kukahikisha hilo amewataka waliobinafsisha viwanda kuhakikisha
kuwa wanawajibishwe kwani alishawahi kusema
nia yake ni kuimarisha viwanda ili watu wafurahie soko la ndani na kuzalisha
ajira nyingi ifikapo 2020.
Akizungumzia kuhusu sekta ya elimu Dk.Magufuli amesema utoaji wa elimu
bure kuanzia elimu ya msingi hadi sekondari ni wenye dhamira ya kweli kwa
serikali yake.
Pia ameahidi kuwa wanafunzi wa elimu ya juu chini ya serikali watapewa
mikopo kwa wakati unaostahili.
Kuhusu
Muungano Zanzibar na Tanganyika Dk.Magufuli amesema ataushughulikia
na kuulinda kwa vile nchi hizo zimeungana zikiwa nchi huru.
Katika hotuba
yake Rais Magufuli amelaani vikali kitendo cha Wabunge wa Vyama vya Upinzani
kuzomea viongozi wa Serikali bungeni na kuwaeleza kuwa hawajakomaa kisiasa na
kuwaita watoto.
“Mmeona tuna kazi kubwa, bado tuna
watoto wengi. Tuendelee kuwavumilia, nadhani na watanzania wameona…… Ndio maana
nimekupongeza sana Mheshimiwa Zitto umekomaa na naamini” amesema rais Magufuli.
Hata hivyo
amewataka wabunge wote kusimama pamoja bila kujali itikadi zao za vyama na
kuacha masuala ya kupigana vijembe, kuzomeana na kutoka nje.
0 comments:
Post a Comment