November 30, 2015


Jeshi la Polisi linawashikilia watu 12 kwa tuhumiwa wa upotevu wa makontena 349 katika bandari ya Dar es Salaam.
Watu hao miongoni mwao ni waliotajwa na Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa na wengine wamebainika kufuatia uchunguzi unaoendelea.
Akitangaza baadhi ya majina hayo Mkurugenzi wa upelelezi wa makosa ya jinai Diwani Athumani amesema baadhi ya majina hayatawekwa hadharani hadi upelelezi utakapo kamilika ili kupeleka watuhumia wote mahakamani.
Akiongea na waandishi wa habari Jijini Dar es salaam Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai amesema uchunguzi unaofanywa na wataalamu waliobobea wa  makosa ya uhalifu wa kifedha umeweza kuwabaini watu hao wamehusika na wizi huo.
Kamanda Athumani amesema kati ya watuhumiwa hao kumi na mbili watano wanashikiliwa na Jeshi la Polisi na saba bado upepelezi unaendelea na utakapokamilika watafikishwa mahakamani.

Wanaoshikiliwa kutokana na tuhuma mbalimbali ni Kamishna wa Idara ya Forodha na Ushuru TRA Tiagi Masamaki, Meneja Kitengo cha Huduma za Ushuru  na Habib Mponezia, Msimamizi Mkuu wa Kitengo cha Ushuru wa Forodha.

0 comments:

Post a Comment