Jumla ya watoto elfu
tatu mia sita na 68 wameanikiwa kutolewa katika ajira mbaya katika kipindi cha
April 2012 hadi sasa Zanzibar.
Kati ya watoto hao
wanawake ni elfu moja mia nne na 98 na wanaume elfu mbili mia moja na 70 kupitia
jumuia TAMWA, KUHAWA, PIRO na COWPZ.
Akizungumza na
waandishi wa habari afisa mradi wa watoto katika wa chama cha waandishi wa
habari wanawake Tanzania TAMWA Sheikha Haji Dau amesema kati ya watoto hao 28
wameacha tena masomo na kurejea tena katika ajira.
Amesema mradi huo
unatarajiwa kuwafikia watoto elfu 5 hadi kukamilika kwake September mwaka huu
chini ya ufadhili wa shirika la save the children.
Afisa Sheikha amefahamisha
kuwa kwa upande wa TAMWA kati ya watoto waliorejeshwa skuli wamekwenda skuli za
msingi na watatu kutoka kijiji cha Chwaka wanasoma kituo cha elimu Mbadala.
0 comments:
Post a Comment