Rais wa Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akifungua kongamano la Ajira. |
Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohammed
Shein amesema serikali imeandaa mazingira bora ya kukabiliana na tatizo la
ajira kwa vijana kwa kuwaongezea vyanzo vya kujiajiri wenyewe.
Amesema tatizo hilo ni changamoto
inayowakabili vijana duniani kote hali inayowafanya kufanya kazi zisizokuwa na heshima.
Dk shein ameeleza hayo alipokuwa
akizungumza katika kongamano la kitaifa la ajira kwa vijana mjini Zanzibar.
Takwimu zainaonyesha zaidi ya
vijana milioni 73 hawana ajira ikiwemo wanaomaliza vyuo vikuu kutokana masomo
wanayomaliza hayaendani na fursa za ajira za sekta rasmi.
0 comments:
Post a Comment