May 19, 2014

Serikali ya Zanzibar imetenga kiasi cha shilingi bilioni 8 kwa ajili ya mradi maalum ya kukabiliana na athari za mabadiliko ya hali ya hewa.
Waziri wa nchi Afisi ya Makamu wa kwanza wa rais Fatma Fereji amesema fedha hizo zitapatikana kupitia mradi wa kuendeleza utalii Zanzibar na zitalenga kuimarisha ustawi wa matumbawe ambayo yamekuwa yakiathiriwa kwa kuongezeka  joto baharini.
Akijibu suala huko baraza la wawakilishi Waziri Fereji amesema tayari utaratibu wa kuanzisha mfuko wa fedha za mabadiliko ya tabia nchi ili  kujikinga na athari zake kwa kuzingatia maeneo muhimu yaliyotajwa kwenye mkakati wa Zanzibar wa mabadiliko hayo.
Amefahamisha kuwa hivi karibuni serikali imejenga kiasi ya matuta mita 1440 kwa baadhi ya maeneo ya kilimo yanayoingia maji ya chumvi ili kupunguza athari za kupanda kwa kina cha bahari.

 

0 comments:

Post a Comment