Akizungumza na waandishi wa habari Waziri
wa afya Juma Duni Haji amesema tayari vipimo
vya wagonjwa hao vimepeleka Dar es salam
kwa uchunguzi zaidi ili kupata
uhakika kama kweli ni ugonjwa huo.
Amesema ugonjwa huo unaoasababishwa na
kirusi cha mbu mweupe (AEDES) anaetafuna mchana umegawika aina tofauti ikiwemo
dengue ya homa, ya damu na ya kupoteza fahamu.
Waziri duni ameongeza kuwa dalili kuu za dengue ni
homa, kuumwa kichwa maumivu ya viungo na uchovu zinazojitokeza kati ya siku 3
na 14 au dalili zinazofanana na malaria.
Amesema mbu huyo huzaliana
katika maji yaliyotuama hasa kwenye vyombo vya nyumbani, kingo za maji ya paa
za nyumba, matairi ya gari, ndoo, vikopo na katika vifaa vidogo vidogo
vinavyotuama maji na tayari wagonjwa kadha wamesharipotiwa jijini dar es
salaam.
Waziri duni amewataka wananchi kuwa waangalifu na kuchukuwa tahadhari ya
kuhakikisha kuwa wanaondoa sehemu zote zinazoweza kuzalisha mbu ikiwemo madimbwi,
vichaka na mashimo ya maji.
Nae Katibu mkuu Wizara ya afya Mohamed Saleh
Jidawi amesema ugonjwa wa Dengue hauna
tiba wala chanjo na unatibiwa kutokana dalili zinazoambatana na ugonjwa huo
ikiwemo kupungukiwa maji au damu.
0 comments:
Post a Comment