May 16, 2014

Bodi ya chakula dawa na vipodozi Zanzibar imesema hali ya uingizaji wa bidhaa za chakula dawa na vipodozi zenye ubora kwa matumizi ya binaadamu nchini inaridhisha.
Mrajis wa bodi hiyo dk burhan Othamn Simai amesema hilo linatokana na mwamko wa wafanyabiashara wengi kufahamu  usalama wa bidhaa hizo kwa watumaiaji.
Hata hivyo amewatahadharisha wafanyabiashara wasiokuwa waaminifu wanaoingiza bidhaa zisizo bora kuwa hatua za kisheria zitachukuliwa.
Akifungua mafunzo ya siku tatu kuhusu utoaji huduma kwa wateja wafanyabiashara wa chakula, dawa na vipodozi  wa nchi za Afrika Mashariki amesema  utoaji wa huduma  bora kutaondoa matatizo mbali mbali ikiwemo maradhi kwa watumiaji.
Mapema mkufunzi wa mafunzo hayo yenye washiriki kutoka Kenya, Uganda, Rwanda Tanzania,  Peter Ssali  kutoka Uganda amesema  ni vyema  nchi za jumuiya ya afrika mashariki kuwa na uwiyano sawa katika kufanikisha huduma za kijamii.

0 comments:

Post a Comment