Jeshi la polisi
linawashikilia wazazi wa mtoto wa Mussa Issa Say kwa tuhuma za kumjeruhi na
pasi katika paja lake la mguu wa kushoto pamoja na kumuathiriwa jicho na kitu
kisichojulikana.
Kamanda wa Mkoa
wa mjini magharibi Mkadama Khamis Mkadama amesema mtoto huyo alifanyiwa ukatili
huo na baba yake mzazi Issa Mazaga Say
kwa madai ya kuiba shilingi 200.
Akizungumza na
waandishi wa habari amesema tukio hilo limetokea tarehe kumi na
tatu mwezi huu huko kilimahewa wilaya ya magharibi unguja.
Amesema jeshi
hilo pia linamshikilia mama wa kambo wa mtoto huyo Khadija Jafar Rashid katika
kituo cha polisi cha Ng’ambo kwa kuchochea vitendo hivyo vya ukatili kwa mtoto
wao.
Kamanda Mkadam
amesema kuwa tayari mtoto huyo ameshapelekwa hospitali Mnazi mmoja kwa matibabu
na jeshi la polisi linaendelea kumpatia matibabu mengine zaidi .
Amewataka wazazi
na walezi kuacha kuwapiga watoto kwa
hasira ili kuepusha madhara kwa watoto hao.
0 comments:
Post a Comment