Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein amesema
wakati umefika kwa Wizara ya Mifugo na Uvuvi kuanza kufikiria uwezekano wa
kuanzisha chuo cha Uvuvi Zanzibar.
Dk.
Shein amesema hayo katika mkutano wa kujadili Mpango kazi na bajeti ya mwaka
2013/14 ya Wizara hiyo kwa kipindi cha miezi tisa kuanzia mwezi Julai 2013.
Amesema
mazingira ya Zanzibar pamoja na mahitaji ya ajira kwa vijana vinalazimisha
kuweko kwa chuo maalum cha uvuvi kitakachosaidia kutoa mafunzo kwa wananchi wa
Zanzibar wanaojihusisha na shughuli za uvuvi wakiwemo vijana.
Amezisisitiza
taasisi za umma zikazingatia thamani halisi ya bei ya bidhaa na huduma
zitakazohitajika wakati wa kupanga na kutekeleza majukumu ya taasisi zao ili
kuwa na bajeti halisi kwa mahitaji halisi.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Dk. Kassim Gharib Juma amesema Wizara amesema
kumekuwa na mafanikio makubwa katika udhibiti wa maradhi yasiyo na mipaka
pamoja na maradhi ya kichaa cha mbwa kutokana na kuimarika kwa huduma za
chanjo.
aidha ameeleza pia sekta ya uvuvi imekuwa na
ongezeko la wavuvi wa baharini ambapo katika
kipindi cha mwaka wa fedha 2013 – 2014 jumla ya tani 23,000 za samaki
zilivuliwa na zimewaingizia wavuvi jumla ya shilingi bilioni 89.7.
0 comments:
Post a Comment