April 02, 2014


Umoja wa Mataifa umeikosoa serikali ya Myanmar kwa kukiuka ahadi ilizotoa kwa  kuwazuia Waislamu wa nchi hiyo kushiriki kwenye sensa ya idadi ya watu.

 Mfuko wa Sensa ya Jamii wa Umoja wa Mataifa (UNFPA) umesema Myanmar iliahidi kuheshimu na kuzingatia viwango vya kimataifa na misingi ya kisheria katika zoezi hilo.

Limeeleza kuwa kutokana na vizuizi vilivyowekwa kwa Waislamu wa kabila la Rohingya inanaitilia  shaka sensa hiyo na inaweza kasababisha kuongezeka mivutano katika mkoa wa Rakhin.

Sensa hiyo ya watu ni ya kwanza kufanyika nchini Myanmar katika kipindi cha miongo mitatu iliyopita, imeanza Jumapili iliyopita na itaendelea hadi April 10.

 Serikali ya Myanmar haiwatambui rasmi Waislamu wa nchi hiyo na hawasaidi  na  mashambulizi ya umwagaji damu yanayofanywa dhidi yao na Mabudha wa nchi hiyo wenye misimamo mikali.

0 comments:

Post a Comment