April 02, 2014



zanjkijiwe.blogspot.com
gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT)  Prof Benno Ndulu
Benki kuu ya Tanzania BOT imezindua taarifa ya matokeo ya utafiti wa matumizi ya huduma za kibenki ulionesha ukuaji wa matumizi ya huduma za kibenki kwa njia ya simu.

Utafiti huo uliofanywa na Mfuko wa kuendeleza sekta ya sera Tanzania katika mikoa ya Tanzania bara na Zanzibar umebaini kuwa takribani kaya elfu nane zinatumia huduma hiyo.  
 Akizindua taarifa hiyo jijini Dar es Salaam Gavana wa BOT Profesa Benno Ndulu amesema utafiti huo hadi umeonesha watu wasiofikiwa na huduma hizo imepungua kutoka  watu milioni kumi na moja hadi  Milioni 6  katika mwaka uliopita.

Amefafanua kuwa tafiti hizo zimebaini kuwa wananchi wengi wameweka akiba katika simu zao  na  wengine hutumia huduma hiyo kwa kulipa malipo mbalimbali ikiwemo umeme na  maji.

Hata hivyo profess Ndulu amesema bado  maeneo mengi ya vijijini hawajafikiw ana huduma za kinenki kikamilifu kutokana na matatizo ya miundo mbinu ya mawasiliano ya ya simu.
huduma za kibenki kwa simuu za kuwa tanzania

0 comments:

Post a Comment