April 02, 2014


Mfanyakazi mmoja wa kike katika Hoteli ya MELIA iliyopo Kiwengwa Mkoa wa Kaskazini Unguja amedai kubakwa na mfanyakazi mwenziwe hotelini hapo.

Akizungumza na vyombo vya habari kwa masikitiko  Neema mwenye umri wa miaka  25 amesema amefanyiwa udhalilishaji huo februari 18 na Nicolas Msambi ambae ni mfanyakazi wa kitengo cha ulinzi katika hoteli hiyo.

“…Ilikuwa majira ya jioni niliombwa na meneja wa ulinzi wa hoteli ya melia kumpika chakula  nyumbani kwake hotelini humo lakini baadae aliniachana Nicolas ambae  alinivamia kwa  nguvu.” Neema ameeleza.

 Uchunguzi umebaini pia mwanamke huyo ameombwa kulipwa fidia ya shilingi milioni mbili kufuta kesi hiyo iliyotokea siku chache baada ya mfanyakazi mwengine wa hoteli ya Melia jina linahifadhiwa kudai kuvuliwa nguo mbele ya wafanyakazi wa kiume kwa madai ya kuiba Dola mbili katika chumba cha mgeni.


Uongozi wa hoteli hiyo umekataa kuelezea juu ya tukio hilo huku kwa waandishi wa habari waliofuatilia tukio hilo.

Jeshi la polisi mkoa wa kaskazini unguja limethibitsha tukio hilo na kueleza linaendelea na upelelezi  wa madai ya kubakwa mfanyakazi huyo wa kampuni ya ulinzi ya security group.

Akielezea tukio hilo Kaimu Kamanda wa polisi Mkoa huo Salma Khamis amefahamisha kuwa wamekusanya sampuli za mtuhumiwa ili  kuchunguza vinasaba jijini Dar es salaammanamke abakwa

kwa upande wake katibu mtendaji wa kamisheni ya utalii amesema tukio hilo linashughulikiwa na Kamisheni ya kazi Zanzibar ambayo pia imesema haihusiki na kesi za aina hiyo

“…….Sisi hatuhusiki na kesi  kama hizo kwa mujibu wa sheria ya kazi Zanzibar tunasimamia migogoro na malamimiko ya wafanyakazi kesi hizo zinashughulikiwa na polisi alifafanua  kamishna wa kamishemni ya kazi Zanzibar.

0 comments:

Post a Comment