April 03, 2014



Jumuiya ya istqama pemba imeshauriwa kuwashirikisha masheha katika zoezi la utambuzi wa mayatima na watoto wenye mazingira magumu wanaotaka kuwasaidia.

Jumuiya hiyo imeanda mradi wa kuwaendeleza kielimu watoto yatima 400 kisiwani humo ili kuondokana na hali ngumu ya maisha.


Akizungumza katkika kikao cha masheha na viongozi wa jumuiya hiyo afisa tawala Mkoa wa Kaskazini Pemba Khamis Salim Mohammed amesema zoezi hilo lita fanikiwa iwapo masheha kwa vile watoto hao wanaishi kwenye shehia zao.


Hata hivyo amewataka masheha hao kuzingatia vigezo utambuzi vinavyohitajika katika utambuzi huo na kuisifu juhudi zinazochukuliwa kusaidia jamii hasa watoto hao wanaoishi katika mazingira magumu pemba.


Nae Kwa upande wake mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Mohammed Suleiman Khalfan ameelezea kusikitishwa na jamii.yatima 400 kusaidiwa pemba

0 comments:

Post a Comment