Shirikisho la Mpira wa
Miguu Tanzania (TFF) limetangaza rasmi Mart Nooij kutoka Uholanzi kuwa kocha
mkuu mpya wa timu ya Taifa (Taifa Stars).
Rais wa TFF, Jamal
Malinzi akimtambulisha kocha huyo leo (Aprili 26 mwaka huu) katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam amesema
anafurahi kumtangaza Nooij na anatarajia Tanzania itanufaika na uzoefu wa kocha huyo hasa katika bara la Afrika.
Nooij kabla ya kupewa mkataba huo wa
kuifundisha Taifa Stars alikuwa na klabu ya St. Georges ya Ethiopia pia amewahi
kufundisha katika nchi za Burkina Faso,
Mali na Msumbiji.
0 comments:
Post a Comment