April 20, 2014

Zaidi ya waislamu elfu tatu kutoka karibu nchi sita wanatarajiwa kushiriki katika Ijitimai kuu ya kimataifa inayotarajiwa kufanyika Juni 16 mwaka huu.
Katibu wa maandalizi ya Ijitimai hiyo Mwalimu Hafidh Jabu amezitaja nchi hizo ni Malawi, Zambia, Rwanda, Kenya, Afrika ya kusini na Msumbiji.
Akielezea maandalizi  Ijitimai hiyo inayofanyika huko fuoni migombani nje ya mji wa Zanzibar.
Amewaomba waislamu kuendelea kutoa michango yao ikiwemo kujitokeza kufanya usafi katika viwanja hivyo.             
 Mwenyekiti wa bodi ya wadhamini wa jumuiya ya Jiisabilillahi Tablighi Markaz Ustadh Vuai Mussa Suleiman amesema wamefanikiwa kujenga kituo hicho cha ijitimai ambacho ni cha kudumu.                                    
Ijitimai hiyo ya kimataifa ya 20 inatarajiwa kufunguliwa na Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Jakaya Kikwete

0 comments:

Post a Comment