Kampuni ya Royal Hanskoning DHV ya Nchini Uholanzi imegundua maeneo ya Fumba, Mangapwani na Maruhubi kuwa ni sehemu nzuri zinazoweza kujengwa bandari za kisasa.
Mkurugenzi wa Kampuni hiyo inayofanya utafiti huo Elzinga Theun amesema hatua za awali zinaonesha maeneo hayo ya Kisiwa cha Unguja ni mazuri kwa Ujenzi wa Babandari kutokana na kuwa na kina kizuri cha maji na kukosekana kwa mawimbi Makali.
Akizungumza katika Semina ya kujadili maendeleo ya Sekta ya Bandari Mjini Zanzibar amefahamisha kuwa ukanda wa mashariki ya unguja ni magumu kujengwa bandari kutokana na Mawimbi makali ya bahari jambo linaloweza kuleta shida
Mkurugenzi Theun ameiomba Serikali ya Zanzibar kutafuta mbinu za kuitanua Bandari ya Malindi ili kuhimili ongezeko la idadi a watumaijai wa bandari hiyo kibiashara .
Kampuni ya Royal Hanskoning DHV ya Nchini Uholanzi inafanya utafiti huo wa kujua maeneo mazuri ya kujenga Bandari katika Visiwa vya Unguja na Pemba unatarajiwa kugharimu Jumla ya Pounds Laki 1.5 za Uengereza zilizolewa na Serikali ya Uholanzi.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano Zanzibar Dkt Juma Malik Akili amesema Serikali inaendelea kufikiria mbinu za kuitanua Bandari hiyo na kukidhi viwango vinavyotakiwa.
Amesema ujenzi wa bandari hizo kutaisaidia Zanzibar kupiga hatua maendeleo na kuufanya uchumi wa Zanzibar kukua kwa kiwango kikubwa.
IMETOLEWA NA MAELEZO ZANZIBAR 03/04/2014
0 comments:
Post a Comment