April 15, 2016

Wazee 21,750 wameanza kunufaika na mpango wa serikali wa utoaji fedha za kujikimu yaani pensheni kwa wazee wote wanaoanzia umri wa miaka 70 ili kuimarisha maisha yao.
Wazee 13,150 ni kutoka Unguja na 8,600 wanatoka Pemba, katika mpango huo, kila mzee atapewa shilingi elfu ishirini kila mwisho wa mwezi.
Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa mpango huo, katibu mkuu wizara ya uwezeshaji, wazee, vijana, wanawake na watoto Asha Ali Abdallah, amesema hatua hiyo ni muhimu kwani nchi nyingi duniani zinao utaratibu kama huo.
Amesema, mbali ya kuwa kufanya hivyo ni wajibu, lakini kunahitaji maamuzi ya kijasiri na utashi wa kisiasa, ambapo serikali ya Zanzibar imeweza kuonesha dhamira yake kuimarisha maisha ya wazee.
Amesema msingi wa pensheni kwa wazee wote wa Zanzibar, ni sera ya hifadhi ya jamii iliyopitishwa mwaka 2014, ukiwa mpango mkuu wa taifa wa dira ya 2020 unaolenga kukuza uchumi na kupunguza umasikini nchini.
Sambamba na hilo alisema kuwa wataendelea kuwa na jukumu kubwa katika kuwasajili wazee wapya watakaokuwa wanaingia katika mpango huo.
Waziri wa fedha Dk Khalid Salum Mohammed, alisema kuwa ili serikali iweze kupata maendeleo ni lazima wafanyakazi na wananchi kuwa wawajibikaji katika utendaji wa kazi zao.
Amesema katika kutekeleza mpango huo watendaji wanapaswa kuwa waadilifu na waaminifu ili kuhakikisha wazee wanaostahi wanapata pencheni zao kama inavyopaswa.
“hali halisi na uzoefu unaonesha kuwa kumekuwa na tabia za udanganyifu na wizi katika masuala mengi yanayohusiana na malipo….lakini nachukua nafasii hii kuwatanabahisha watendaji wote watakaohusika na utekelezaji wa mpango huu katika ngazi zote yoyote atakaebanika kufanya udanganyifu hatua kali zinatuchukuliwa dhidi yake” amesema.
Aidha amewataka watendaji wa mpango huo kuwa na  hekima, busara, uvumilivu, upole na huruma ni lazima zichukue nafasi yake katika kuwahudumia wazee.
Nae waziri wa Kazi,uwezeshaji,wazee,vijana,wanawake na watoto Moudline Castico ameahidi kwamba mpango huo utasimamiwa kwa nguvu zote ili kuhakikisha wazee wote wanaostahiki wanapatiwa fedha zao kwa wakati na hakutakuwa na udanganyifu na upotevu wa fedha za serikali.
Mpango huo unatarajiwa kutumia shilingi miioni 435 kwa mwezi ambapo ni sawa na shilingi bilioni 5.220 kwa mwaka.
Zanzibar inakuwa nchi ya kwanza Afrika mashariki kuanzisha mpango huo, nay a sita kwa Afrika baada ya Mauritius, Afrika Kusini, Lesotho, Namibia na Botswana.

Waziri wa Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Vijana, Wanawake na watoto
Moudline Castico akielezea mikakati yao yakuwasaidia wazee
katika hafla ya uzinduzi wa mpango wa pencheni kwa Wazee wa Zanzibar
 (kulia) Waziri wa Fedha na Mipango Zanzibar Khalid Salim Mohammed.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazee Zanzibar Aboud Talib Aboud
akisoma risala ya wazee kwa mgeni rasmini
Waziri wa Fedha na Mipango Zanzibar Khalid Salim Mohammed.
Waziri wa Fedha na Mipango Zanzibar Khalid Salim Mohammed
akimkabidhi pencheni Bi. Erestina Filex katika uzinduzi wa mpango
wa pencheni kwa wazee wa Zanzibar uliozinduliwa leo April 15/2016






Maelezo Zanzibar.

0 comments:

Post a Comment