April 15, 2016

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imesema haitafumbia kufumbia macho matukio ya uchomaji moto wa nyumba unaoaminika kauwa wa kimazingara katika kijiji cha koani kibondemaji.   
Akizungumza katika ziara ya kutembelea eneo hilo Waziri wa nchi afisi ya Makamo wa pili wa Rais Mohamed Aboud Mohamed amesema tukio hilo limekuwa likiwakosesha watu amani na kuwaongezea umasikini.
Amesema serikali iko tayari kutumia mbinu zozote kwa kushirikiana na wakaazi wa eneo hilo pamoja na vyombo vya ulinzi na usalama kulipatia ufumbuzi tatizo hilo pamoja na kujua chanzo halisi cha mkasa huo wa kushangaza.
Mh aboud ambae alishuhudia moto huo ukiwaka katika nyumba mbili kwa wakati tofauti na amewataka wananchi kuwa wastahamilivu kwa kuelewa kuwa huo ni mtihani unaowakabili kwa kipindi hiki.
Nyumba hizo zinazokadiriwa kufikia saba zenye wakaazi 39 zimeanza kuchomwa moto tokea 4 April 2016 ambapo tayari wakaazi wa nyumba hizo wameathirika baada ya mali zao kadhaa kuchomwa moto.        
Akielezea tukio hilo sheha wa Shehia ya Koani Kibondemaji B Tunza Ali Shaali amesema moto huo umekuwa ukiwaka bila ya kutegemewa na mara nyingi hutokea pale nyumba inapokuwa haina mtu hali inayowafanya kushindwa kuendelea na kazi zao za kawaida.
Katika ziara hiyo Wazri  aboud amewakabidhi wananchi hao walioathirika na tatizo la kuunguliwa kwa nyumba zao vifaa mbali mbali vikiwemo magodoro, mchele, sukari na vifaa vya nyumbani pamoja na fedha taslim kutoka Kamisheni ya kukabiliana na Maafa Zanzibar.
Wakati huo huo Waziri  Aboud mohamed amelitaka jeshi la polisi kuhakikisha hadi Jumatatu 18 April  wanatoa taarifa juu ya uchunguzi kwa watu waliohusika na uchafuaji wa maji katika huko Bububu.
Amesema jambo hilo si la kuvumiliana na kuoneana muhali kwa vile linawagusa watu wote na ni kinyume na ubinadamu hivyo ni lazima kwa polisi kuchukua hatua hizo haraka.
Mh Aboud ameeleza hayo alipokuwa akizungumza na wananchi walioathirika na uchafuzi wa maji ya zawa baada ya kutiwa mafuta machafu (mobile mchafu) wiki  iliyopita .
Amesema serikali kwa sasa haiwezi kuvumilia vitendo hivyo kwani vitendo hivyo ambavyo vinarejesha nyuma juhudi za serikali za kuwapatia wananchi huduma hiyo.
 Pia Waziri Aboud pia ametembelea ghala la kuhifadhia vifaa vya maafa Saateni pamoja na kuangalia maendeleo ya ujenzi wa jengo  la  afisi ya Kamisheni ya Kukabiliana na Maafa Zanzibar.
Akizungumza katika ziara hiyo Mkurugezi Mtendaji wa Kamisheni hiyo Ali Juma Hamadiamesema jengo hilo litakuwa ni kituo kipya cha operesheni za taasisi hizo ambayo itakuwa na ofisi pamoja na ghala lakuhifadhia vitu mbali mbali vya maafa.

Waziri wa nchi Afisi ya Makamu wa pili wa Rais Mohamed Aboud Mohamed
akiangalia moja ya kisima maji yake yaliyoathirika na mafuta hayo machafu huko
Bububu nje ya Mji wa Zanzibar

Mkurugenzi mtendaji wa Kamisheni ya Kukabiliana na Maafa Zanzibar akimtembeza
 Waziri Aboud kuangalia maendeleo ya ujenzi wa afisi ya taaisisi hiyo huko Maruhubi
nje kidogo ya Mji wa Zanzibar


0 comments:

Post a Comment