Umoja wa Vyama visivyo na wakilishi Bungeni
umewaomba wananchi wa Zanzibar kushiriki uchaguzi wa marejeo wa Jumapili ijayo
kwa hali ya amani na utulivu ili kila moja aweze kutumia haki yake ya msingi.
Umesema kuwa hiyo ndio fursa pekee ya
kuwapata viongozi wapya watakao uongoza nchi kwa kipindi cha miaka mitano.
Wakizungumza
na waandishi wa habari juu ya ushiriki wao katika uchaguzi mwenyekiti wa umoja
huo Ali Kaniki amesema kurejewa uchaguzi kusiwe chanzo cha machafuko ya
kisiasa nchini hasa kwa wale
wasiotakia mema taifa.
Amesema vyama hivyo vimeamua kushiriki
uchaguzi huo wa marejeo na hawana
pingamizi na maamuzi yaliyotolewa na tume ya uchaguzi Zanzibar kwa kuwa ule wa
awali ulifutwa kisheria.
Amesema chama chochote cha siasa kazi yake
ni kushiriki uchaguzi na sio kususia kwani kufanya hivyo kutakosesha wananchi
haki yao ya msingi na kurudisha nyuma shughuli za maendeleo.
Nae katibu mkuu wa umoja
huo Rovatus Muabhi amefahamisha
wamechukuwa maauzi hayo kwa
mujibu wa sheria ya nchi na ni tofauti na inavyotangazwa kuwa wamerubuniwa na
vyama vyengine vya kisiasa.
Makatibu hao wamesema kurejewa uchaguzi
sio jambo geni duniani na yapo mataifa mengi yamewahi kurejea uchaguzi
kutokana na kasoro mbali mbali zilizojitokeza katika chaguzi zao.
Viongozi wa Umoja huo
wamesema pamoja na kushiriki uchaguzi pia wamesimamisha wagombea
12 ambao wamo katika ngazi zote ikiwemo rais, wawakilishi na madiwani.
Vyama hivyo ni pamoja na vitakavyoshiriki
katika marudiao ya uchaguzi huo ni DP, CCK, AFP, DEMOKRASIA MAKINI, SAU, TLP,
UPDP, UMD, ADC, NRA, TADEA NA CHAUMMA.
Mmoja wa wagombea Urais kwa tiketi ya chama cha TLP Hafidh Hassan Suleiman
akithibitika wa kugombea na kuwataka wananchi kumpikia
kura yeye.
Picha Maelezo Zanzibar
|
0 comments:
Post a Comment