Tume ya Taifa
ya Uchaguzi (NEC),imesema haitambui kujitoa kwa Chama cha Wananchi
(CUF),katika uchaguzi wa Mbunge Jimbo la Kijitoupele hapa Zanzibar
unaotarajiwa kufanyika Jumapili licha ya kuwa Tume imepokea barua rasmi
toka kwa uongozi wa Chama hicho.
Mkurugenzi wa
uchaguzi wa Tume ya Taifa Bw Kailima Ramadhani amesema Tume imefikia maamuzi
hayo kutokana na ukweli kuwa barua hiyo ya CUF imechelewa huku maandalizi ya
uchaguzi huo yakiwa yamekamilika na ni Wananchi tu kwa sasa Wanasubiriwa kwenda
kupiga kura.
Aidha Bw Kailima
ameeleza kuwa,kwa kuwa karatasi za kupigia kura zilishachapishwa na kuwasili
hapa nchini tayari kwa uchaguzi huo,zitaendelea kuwa na picha za Wagombea wa
CUF hata kama wamejitoa katika uchaguzi huo.
Awali,wajumbe wa Tume
ya Taifa ya uchaguzi wakiongozwa na Makamu Mwenyekiti wa Tume Jaji
mstaafu Hamid Mahamood Hamid walitembelea katika vituo mbalimbali vya
kupigia kura katika Jimbo la Kijitoupele ili kujiridhisha na maandalizi ya
uchaguzi huo kabla ya uchaguzi kufanyika jumapili.
Tume ilibaini kuwepo
kwa baadhi ya kasoro ndogondogo katika baadhi ya vituo vya kupigia kura ikiwa
ni pamoja na kubanduliwa kwa karatasi zenye majina ya wapiga kura,mfano katika
kituo cha Skuli ya sekondari Kinuni.
Jimbo la Kijitoupele
lina jumla ya Wapiga kura wapatao 17,274 na vituo vipatavyo 53 vitatumiwa na
wapiga kura ili kumchagua mbunge wa Jimbo la Kijitoupele siku ya Jumapili.
Sambamba na Uchaguzi
wa ubunge katika Jimbo la Kijitoupele, marudio ya uchaguzi mkuu wa Zanzibar
Oktoba 25,2015 ambayo matokeo yake yalifutwa uatafanyika Jumapili hiyo pia.
Uchaguzi katika jimbo
la Kijitoupele uliahirishwa mwaka jana kutokana na hitilafu ndogondogo
zilizojitokeza katika karatasi za kupigia kura,kabla ya kufutwa kwa matokeo ya
Uchaguzi mkuu wa Zanzibar uliofanyika Oktoba 25,2015.
Clarence Nanyaro- NEC
0 comments:
Post a Comment