Umoja wa vijana wa CCM (UVCCM) umesema
uchaguzi wa marudio unaotarajiwa kufanyika Jumapili ya Machi 20 mwaka huu ndiyo sululisho
la kutatua mvutano wa kisiasa uliopo nchini.
Umesema mvutano huo uliotokea baada ya Tume ya
uchaguzi Zanzibar ZEC kufuta matokeo utatatuliwa kwa njia ya kidemokrasia baada
ya kufanyika uchaguzi huru na wa haki utakaofanikisha kupatikana viongozi
watakaoweza kuongoza dola kwa miaka mitano ijayo.
Akizunguza na waandishi wa habari Kaimu Katibu
Mkuu wa UVCCM, Shaka Hamdu Shaka amesema malumbano, vurugu na vitisho kwa
sasa havina nafasi bali wanasiasa waungane na kuwa wamoja kwa kuwahamasisha
wananchi wenye sifa kutekeleza haki yao ya kidemokrasia na waliokuwa hawashiriki
wasiwazuie watu wengine wanaotaka kupiga kura .
Amewataka wananchi kuchambua kwa kina hoja na
mijadala inayojengwa na wanasiasa juu ya hatima ya maendeleo ya Zanzibar kisha
wafanye maamuzi ya kuchagua viongozi wanaohisi wanafaa kuongoza dola.
Amesema kwa sasa kuna baadhi ya makundi ya watu
wanaotumia mitandao ya kijamii kusambaza uongo kuwa hali ya Zanzibar sio shwari
wakati si sahihi.
Amesema ni vyema suala hilo kukemewa na
wanaharakati kabla hazijaleta athari kwa nchi.
0 comments:
Post a Comment