Viongozi wa Umoja wa Rufaa za Wananchi
Tanzania umewaomba Wazanzibari kwenda kukamilisha haki yao ya kidemokrasia ya
kupiga kura kwa kuwachagua Viongozi wanaowataka kuwaletea maendeleo
kwenye uchaguzi Mkuu wa marejeo wa Zanzibar unaotarajiwa kufanyia Jumapili ya
Tarehe 20 mwezi huu.
Kauli hiyo imetolewa na
Ujumbe wa Viongozi saba wanaotoka vyama vidogo vidogo vya
Kisasa Nchini Tanzania vilivyokuwa havimo kwenye Umoja wa Ukawa
ukiongozwa na Mhe John Shibuda wakati walipokutana kwa mazungumzo na Makamu wa
Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Ofisini kwake Vuga Mjini
Zanzibar.
Shibuda alisema
kinachohitajika wakati huu kwa Taifa ni kuona watanzania wanaendelea kuishi kwa
amani na ushirikiano utakaotoa nafasi pana kwa Wananchi wake kujikita zaidi
katika uzalishaji mali badala ya kuhubiri Siasa.
Aliipongeza Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar kwa kushirikiana na ile ya Jamuhuri ya Muungano wa
Tanzania kupitia vikosi vyake vya ulinzi kwa kulinda amani ya Zanzibar.
Shibuda aliwataka
Wanachama wa vyama vya siasa, Viongozi pamoja na Wananchi kukamilisha zoezi la
kupiga kura kwa amani na usalama ili lengo la kurejewa uchaguzi huo likamilike
na kuleta mafanikio makubwa.
Alitahadharisha kwamba si
vyema wakati wa uchaguzi wakajitokea baadhi ya watu kutaka kuchezea
matokeo ya kura jambo ambalo ni hatari na matokeo yake ni kwamba gharama za
kuja kulinda vurugu ni ndogo.
Naye Mjumbe wa Umoja huo
wa Rufaa za Wananchi Tanzania John Momos Cheo alisema upigaji kura ya
marejeo Jumapili ijayo ndio njia pekee itakayotoa mwanga kwa Wananchi wa Visiwa
vya Zanzibar kuamua wapi wanataka kuelekea katika mustakabali wa maisha yao ya
baadaye.
Akitoa shukrani zake
kwa Ujumbe huo wa Umoja wa Rufaa za Wananchi Tanzania, Makamu wa Pili wa
Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema Tume huru ya Uchaguzi Zanzibar {
ZEC } haikufanya makosa kufuta uchaguzi Mkuu wa Zanzibar wa Tarehe 25 Oktoba
mwaka 2015.
Balozi Seif alisema yapo
mambo tisa yaliyoainishwa na Mwenyekiti wa Tume hiyo Jecha Salum Jecha ambayo
yalichangia kuvuruga zoezi zima la uchaguzi na kufikia hatua ya kufuta
uchjaguzi pamoja na matokeo yake yote.
Makamu wa Pili wa Rais wa
Zanzibar aliuhakikishia Ujumbe wa Viongozi hao wa Umoja wa Rufaa za Wananchi
Tanzania kwamba Serikali itaendelea kusimamia amani ili kuona zoezi hilo
la uchaguzi linakamilika kwa utulivu.
Balozi Seif alisema
jukumu hilo la Serikali limelenga kuona Maisha ya kila siku yanatoa nafasi kwa
Wananchi waendelee kufanya shughuli zao za kimaisha kama kawaida.
Ujumbe huo wa Umoja wa Rufaa za Wananchi uliofanya ziara ya siku mbili Zanzibar umejumuisha Viongozi wa Kisiasa wa vyama visivyokuwa ndani ya Ukawa vya UPDP, SAU, UDP na ADATADEA.
Ujumbe huo wa Umoja wa Rufaa za Wananchi uliofanya ziara ya siku mbili Zanzibar umejumuisha Viongozi wa Kisiasa wa vyama visivyokuwa ndani ya Ukawa vya UPDP, SAU, UDP na ADATADEA.
0 comments:
Post a Comment