Umoja wa vyama visivyo
na uwakilishi bungeni vimethibisha
kushiriki uchaguzi Mkuu wa marudio wa Zanzibar utakaofanyika Jumapili
ijayo ya Machi 20.
Vyama hivyo ni pamoja na DP, CCK, SAU, AFP, TLP, ADA TADEA,
UPDP, D. MAKINI, NRA, UMD, CHAUSTA NA ADC.
Uthibitisho huo umetolewa jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu
wa chama cha Democraty Party (DP) Abdul Mluya kwa niaba ya mwenyekiti wa
makatibu wakuu wa umoja huo.
Akizungumza na waandishi wa habari amesema wamefikia hatua
hiyo kutokana na vyama vyao kuitambua
tume ya uchaguzi ya zanzibar (ZEC) ndio chombo pekee chenye mamlaka ya
kutangaza tarehe ya uchaguzi kwa mujibu ya sheria na katiba ya Zanzibar ya 1984.
“kwa kuwa vyama hivi vilishiriki uchaguzi wa
rais Oct 25, 2015 vikiwa na imani na Tume ya Uchaguzi kwa imani hiyo ndio maana vyama hivi
vilishiriki uchaguzi huo wa awali, hivyo hatunabudi kushiriki uchaguzi wa
marejeo ili demokrasia ishike mkondo wake na mshindi apatikane”. amesema Abdul MluyaAmewaomba wananchi wa Zanzibar kujitokeza kwa wingi siku ya
uchaguzi ili kuamua hatma yao kwa miaka mitano ijayo na kuliomba jeshi la
polisi kusimamia amani pamoja na uchaguzi ili uwe wa amani.
Nae
katibu mkuu wa umoja huo Rovatus Muabhi amewataka mabalozi, taasisi na
mashirika ya kimataifa kuacha kuingilia masuala ya siasa nchini kwa vile Zanzibar
ni nchi na matatizo yaliyopo yatatatuliwa na wazanzibari wenyewe.
0 comments:
Post a Comment