Jeshi la Polisi Zanzibar linawashikilia watu 42
wakituhumiwa kuhusika na mlipuko uliotokea juzi usiku katika nyumba ya Kamishna
wa Polisi, Hamdan Omar Makame.
Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi
za makao makuu ya polisi Ziwani, Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Mjini Magharibi,
Mkadam Khamis Mkadam alisema hadi jana mchana watu 42 walikuwa ndani kwa ajili
ya kuhojiwa na jeshi hilo.
Alisema uchunguzi unaendelea na bado watu
wengine wanatafutwa kuhusiana na tukio hilo.
“Bado tunaendelea na uchunguzi wa jambo hili na tukishakamilisha tutatoa taarifa rasmi,” alisema Kamanda Mkadam.
“Bado tunaendelea na uchunguzi wa jambo hili na tukishakamilisha tutatoa taarifa rasmi,” alisema Kamanda Mkadam.
0 comments:
Post a Comment